Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amesema kikosi chake kinapaswa kujiangalia kwenye kioo baada ya matumaini yao ya kuwania ubingwa wa England msimu huu kufifia.

Arsenal ilikubali kipigo cha mabao 4-1 toka kwa Manchester City katika Uwanja wa Etihad kwa mabao mawili ya Kevin De Bryune, John Stone na Erling Haaland kila mmoja akifunga bao moja na Rob Holding akiifungia Arsenal bao la kufutia machozi.

City imepunguza tofauti ya alama mpaka kufikia alama mbili dhidi ya Arsenal ambao pamoja na kufungwa bado wanaongoza ligi hiyo ingawa City wana michezo miwili mkononi.

“Tathmini iko wazi, timu bora imeshinda mechi, pengine walikuwa kwenye kiwango bora sana, hasa kipindi cha kwanza na hatukuweza kufikia ubora wao. Wakati hilo likitokea tofauti ikawa kubwa sana,” amesema Arteta.

“Tumepoteza mechi lakini lazima tukubali tumepoteza kwa namna tofauti na jinsi tulivyopoteza mchezo tuliocheza Emirate dhidi ya Man City. Ubora wa kiwango ulikuwa na tofauti kubwa kati ya timu moja na nyingine.”

Mchungaji mponya Ukimwi apandishwa kizimbani
Xavi ashindwa kujitetea FC Barcelona