Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta ameimwagia sifa kedekede timu yake baada ya kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kwa kuifunga Lens mabao 6-0, Jumatano (Novemba 29) kaskazini mwa London.

Ushindi wa Washika Bunduki hao ulikuwa ni mkubwa zaidi kuupata kwa timu ya England dhidi ya wapinzani wa Ufaransa katika mashindano ya Ulaya.

“Sikuwa na ndoto kama hii,” alisema Arteta akiwaambia waandishi wa habari.

“Tulikuwa na nafasi ya kufuzu na kuwa vinara wa kundi na nadhani tumefanya hivyo kwa njia ya kuridhisha.

“Timu tangu mwanzo ilionyesha kiwango na dhamira onyesha kiwango ya kushinda mchezo. Kila kitu kilifanyika kwa njia sahihi katika dakika 30 za kwanża.”

Arteta alisema timu yake imekuwa ikionyesha hali kama hiyo nyumbani kwa muda, na anakaribisha ukweli wachezaji sita tofauti walikuwa na majina yao kwenye karatasi ya matokeo.

“Uthabiti ambao tumeonesha nyumbani kwa kutoruhusu bao lolote na kufunga ni jambo chanya,” alisema.

“Sasa tusubiri. Tutajua Februari tunakabiliana na nani katika raundi inayofuata na tuone jinsi tulivyo katika wakati huo.

Melis Medo: Wachezaji Dodoma Jiji wameridhika
Ally Kamwe: Al Ahly itatupandisha viwango Afrika