Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta amefichua kuwa amefikiria kuwabadilisha makipa wake, Aaron Ramsdale na David Raya, katika michezo ya karibuni.
Hali ya mlinda mlango wa Arsenal imekuwa gumzo miongoni mwa mashabiki tangu klabu hiyo ilipofanya uamuzi wa kumsajili David Raya aliyetua kwa mkopo kutoka Brentford wakati wa majira ya joto.
Ramsdale alishikilia nafasi ya kuanza kwa mechi nne za kwanza za msimu wa Ligi Kuu ya England, hata hivyo Raya hatimaye alipangwa katika mchezo wa Arsenal na Everton juzi Jumapili (Septemba 17) mchezo ambao walishinda bao 1-0 pale Goodison Park.
Baada ya ushindi huo, Arteta aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa kumuanzisha Raya mbele ya Ramsdale.
“Mawazo yale yale ambayo Fabio Vieira alicheza hapa au Eddie Nketiah alicheza badala ya Gabriel Jesus. Sijawa na swali hata moja kwa nini Gabriel Jesus hajaanza. Ameshinda mataji mengi zaidi ya mtu yeyote, nikiwamo mimi.
“Ni kitu ambacho kimefanywa kihistoria kama hiki, lakini siwezi kuwa na wachezaji wawili kama hawa katika nafasi moja na nisiwacheze. David ana sifa nzuri kama vile Aaron anazo.”
Arteta aliendelea kusema kwamba alifikiria kuwabadilisha makipa wake katika mechi za hivi karibuni akikiri kwamba “najuta” kwa kutofanya hivyo.
“Iko hivi. Mimi ni kocha mchanga sana. Nimekuwa kwenye kazi hii kwa miaka mitatu na nusu na sijutii kwa kile nilichokifanya.
“Mojawapo ni kwamba katika nyakati mbili, nilihisi dakika 60 na dakika 85, katika michezo miwili, katika kipindi hiki, kubadilisha kipa katika wakati huo. Lakini sikufanya hivyo. Sikuwa na ujasiri wa kufanya hivyo.
“Lakini nina uwezo wa kuchukua winga au mshambuliaji, au beki wa kati juu ya kushuka hadi tano na kushikilia matokeo hayo.
“Tulitoka sare kwenye michezo hiyo na sikuwa na furaha. Hiyo ni ajabu? Kwa nini? Tuna sifa zote kwa kipa mwingine kufanya kitu wakati kitu kinatokea na unataka kubadilisha kasi.
“Sasa hisia zangu ni kumfanya kila mtu ashiriki katika timu. Wanapaswa kucheza, bila kujali ushindani. Lazima tufanye hivyo. Huu ni ujumbe wangu.”