Magereza 10 yaliyoteuliwa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kulitaka Jeshi la Magereza litumie rasilimali watu ya wafungwa kuanzisha mazao kwa ajili ya biashara na chakula, badala ya Serikali kuingia gharama ya kulisha wafungwa yametajwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni.
Akizungumza alipotembelea Gereza la Kwamgumi Wilayani korogwe mkoani Tanga, Masauni amesema utekelezaji wa agizo la Rais umeamua kwenda sambamba na uteuzi wa magereza 10 ya kilimo nchini na ameweka wazi mpango maalumu wa kutathimini na kupima mpango mkakati huo kwa kila gereza.
Mikoa ambayo magereza yake yatahusika na kilimo cha Mahindi ni, Mbeya Gereza la (Songwe),Ruvuma (katai), Njombe (ludewa) ,Rukwa (mollo), Kagera (kitengule).
kwa upande wa mikoa ambayo magereza yake yameteuliwa kulima Maharage ni Gereza la Arusha, Rukwa (Kitete), Kagere (kitengule), na kwa magereza mawili ya Morogoro kulima Mpunga ambayo ni, Idete na Gereza la Kiberege.
Mkuu wa Gereza la Kwamgumi, Christopher Mwenda, amesema wao kama uongozi wa gereza hilo wamejipanga vizuri katika utekelezaji wa agizo hilo huku akiiomba Wizara kuongeza vifaa vya Kilimo.