Polisi Nchini Malawi wamewakamata wananwake wawili wenye umri kati ya miaka 20 baada ya kutumia noti za Kwacha kama kama mapambo ya keki iliyookwa na kuiweka kwenye mitandao ya kijamii.
Msemaji wa Polisi nchini humo amesema kuwa wawili hao walichapisha picha ya keki hiyo kwenye mitanda ya kijamii walipokuwa wakitangaza biashara yao ya kuuza keki ambapo keki hiyo imepambwa kwa noti 70 za 500 za Kwacha zenye thamani ya $35.
Hata hivyo Polisi nchini humo wamesema watashtakiwa kwa kosa la kuharibu na kutumia fedha kinyume cha sheria.
Benk Kuu ya malawi imesema inaingia gharama kubwa kuchapisha noti mpya kuchukua nafasi ya zilizochakaa na kulaumu matumizi yasiyofaa ya noti kama moja ya sababu noti hizo kubadilishwa mara kwa mara.