Imeelezwa kuwa, akina mama takribani Milioni 2 hujifungua kabla ya umri wa mimba kukamilika Nchini, ambapo kati ya hao 220,000 hupata watoto waliozaliwa chini ya wakati ikiwa ni sawa na asilimia 11 wanaojifungua kabla ya umri wa mimba kukamilika kila mwaka.
Hayo yamebainishwa mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Hospital ya Benjamini Mkapa (BMH), Alphonce Chandika katika siku ya Maadhimisho ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati Duniani yaliyoeba kauli mbiu isemayo “Vitendo kidogo matokeo makubwa.”
Amesema, hali hiyo ya Mama kujifungua Mtoto kabla ya muda inasababishwa na lishe duni kwa mama, upungufu wa damu pamoja na kukosekana kwa vitamini muhimu zinazohitajika kwenye mwili wa Mama na kwamba zaidi ya Watoto chini ya siku 28 sawa na asilimia 27 hufariki Dunia kwa kuzaliwa kabla ya wakati.
“Kwa upande yetu idadi hiyo ni kubwa na ndiomaana Serikali yetu ya awamu ya sita imewekeza miundo mbinu, dawa vifaa tiba na kuhakikisha watumishi wetu wanaudhuria mafunzo mbalimbali ya kuongeza ujuzi,” amesema.
Hospitali hiyo ya Benjamini Mkapa inaendelea na huduma ya kuwaokoa watoto waliozaliwa wakiwa na utumbo nje, ambapo .paka sasa Watoto watano kati ya15 waliokuwa wamelazwa wameruhusiwa.