Muigizaji maarufu wa Hollywood, Mila Kunis amethibitisha tetesi zilizosambaa hivi karibuni kuwa amefunga ndoa na Ashton Kutcher.

Akiongea katika mahojiano na Jarida la The Telegraph, Kunis alijimtaja Ashton kama mume wake wakati akielezea maisha yao, kauli ambayo hakuwahi kuitoa awali.

“My husband is an incredibly hands – on dad,” alisema Kunis. “When my child was born, I was breast-feeding and he said, ‘That’s your connection,’aliongeza.

Oktoba, 2014, Kunis na Kutcher walipata mtoto wao wa kike, Wyatt. Waigizaji hao wakubwa walidaiwa kufunga ndoa kimyakimya mwezi Machi mwaka huu.

Mila Kunis alipoulizwa katika show ya ‘Late Late Night’ mwezi huo wa Machi, kama kweli alifunga ndoa na Ashton alijibu, “may be”. Hivyo, hii ni mara ya kwanza anathibitisha kwa kumuita muigizaji huyo wa kiume ‘mume wangu’.

Mrembo huyo pia alieleza kuwa yeye na mumewe wanamiliki bunduki ndani ya nyumba yao. Alisisitiza kuwa ingawa wana mashine hiyo ndani ya nyumba hawataruhusu mtoto wao aiguse atakapokuwa mkubwa.

Audio: Drake Ashiriki Kwenye Remix Ya Ojuelegba Ya Wizkid
Tanzia: Mzee Ojwang Wa Vitimbi Afariki