Wizara ya Maliasili na Utalii, imesema vitendo vya ujangili nchini vimepungua kwa mwaka uliopita ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Aidha kupungua kawa ujangili kumetokana kuwapo kwa ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama, mamlaka husika na wananchi katika kutoa taarifa na kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu wa ujangili wa tembo.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gaudence Milanzi alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha mafunzo ya siku tano kwa watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) na wakuu wa mapori ya akiba.
 “kazi ya sasa kwa mamlaka kwa kushirikiana na nyingine ni kazi ya kuhakikisha majangili hawawezi tena kuingia ndani ya mapori ya hifadhi kwa ajili ya kuua wanyamapori hasa tembo, na hii itasaidia kukomesha biashara hii haramu,” amesema Milanzi.
Hata hivyo, amesema licha ya kupungua kwa ujangili tofauti na miaka ya nyuma, lakini bado unaendelea kufanyika kwa kiwango kidogo na kutokana na hali hiyo juhudi za pamoja zinahitajika katika suala la ukamataji na udhibiti kwenye maeneo ya hifadhi za taifa.

Ni Patashika Nguo Kuraruka, Nani Kukosa Usingizi Leo?
FIFA Kuongeza Timu Shiriki Fainali Za Kombe La Dunia