Mwimbaji wa zamani wa Disney princess, Miley Cyrus ametangaza kuwa mshereheshaji wa tuzo za video, MTV Video Music Awards, zitakazo fanyika mwishoni mwa mwezi Agosti.

Miley ametoa tangazo lake kupitia Twitter akiwa amevaa mavazi ya rangi ya kijani yenye maandishi yanayotoa jumbe mbili tofauti.

Ujumbe wa kwanza unagusa kitendo cha waandaaji wa tuzo hizo kumnyima nafasi ya kuperform kwenye tuzo za mwaka jana.Uamuzi huo ulitokana na jinsi ambavyo ‘Miley Cyrus’ alijitoa ufahamu wakati anaperform kwenye tuzo za mwaka 2013 na ku-twerk mbele ya Robin Thicke kama wako faragha.

Mtindo huo uliwafanya watu kubaki mdomo wazi huku watoto wa Will Smith, Jaden na Willow wakiwakilisha kundi la watoto ambao hawakutakiwa kuona kitendo kile.

Itakuwa vipi mwaka huu ambapo msanii huyo mwenye vituko tata atapewa nafasi ya kuonekana mara kwa mara nyingi kwenye jukwaa la tuzo hizo akiongoza ratiba?

Mwaka jana, Miley Cyrus alishinda tuzo kubwa ya video ya mwaka kupitia wimbo wake ‘Wrecking Ball’.

Ciara Ayapotezea Malalamiko Ya Future
Jokate Ajuta Kumfahamu Diamond