Milionea kutoka Jamhuri ya Czech Radim Passer anachunguzwa na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Ujerumani kwa kuendesha gari yake kwa kasi zaidi.
Mmiliki huyo wa gari aina ya Bugatti Chiron alichapisha video ya jinsi alivyoongeza kasi hadi kilomita 417 kwa saa kwenye gari lake kwenye barabara moja katika eneo la Saxony-Anhalt nchini Ujerumani msimu uliopita wa joto .
Sheria ya ujerumani inasema hakuna kikomo rasmi cha kasi kwa magari lakini ikiwa ofisi ya mwendesha mashitaka wa jiji la Stendal atapata uhalifu katika vitendo vyake, anaweza kufungwa jela miaka miwili, au angalau faini kubwa.
Hali hiyo imezidishwa kuwa mbaya baada ya kugundulika kwamba mnamo 2015 Passer tayari alikuwa akiongeza kasi kwenye barabara moja ya nchi hiyo hadi kilomita 400 kwa saa katika Bugatti Veyron.
Mara zote mbili alichapisha video kwenye mtandao wa YouTube, na zimetazamnwa zaidi ya mara milioni 10.
Waziri wa Uchukuzi wa Ujerumani Volker Wissing alilaani tabia ya dereva huyo akibainisha kuwa ingawa hakuna vizuizi vya mwendo kasi kwenye barabara za magari, gari lazima liwe na udhibiti kila wakati.