Mtoto mmoja wa kike kutoka Australia anaelekea kustaafu akiwa milionea katika umri wa miaka 15 licha ya kuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi.
Mtoto huyo, Pixie Curtis mwenye miaka 10 alianzisha kampuni ya midoli ambayo inamuongizia kiasi kikubwa cha pesa ambacho kinakidhi mahitaji ya familia yake yote.
Kwa msaada wa mama yake, Roxy Jacenko, Pixie aliweza kuanzisha kampuni yake inayoitwa Pixie’s Fidget ambayo aliizindua mwaka uliopita na kuuza midoli yote ndani ya saa 48.
Mbali na hilo, Pixie ana kampuni nyingine ya vifaa vya nywele inayoitwa Pixie’s bow, ambayo mama yake aliianzisha wakati akiwa mtoto.
Kampuni zote hizi ni sehemu ya Pixie’s Pix, ambayo pia inauza vifaa vya michezo ya watoto na amekuwa akitoa misaada kwa nyakati tofauti na kwa wahitaji tofauti tofauti.
Mama yake amesema mwanawe anaweza kustaafu akifikisha umri wa miaka 15 endapo atataka kufanya hivyo.
Jacenko ambaye ni mama wa Pixie, ni mmiliki wa biashara mbalimbali ambazo zinafanya vizuri ikiwemo kampuni ya Sweaty Betty PR.