Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) imetenga kiasi cha shilingi milioni 10 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa aliyekuwa mhasibu wa Taasisi hiyo, Godfrey Gugai.
Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Bregadia Jenerali, John Mbungo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa mtumishi huyo awali alionyesha ushirikiano wa kujibu tuhuma zilizokuwa zikimkabili lakini ghafla alitoweka.
“Alielekea kuonyesha ushirikiano lakini alipoona hana maelezo ya namna gani alizipata hizo mali akaamua kukimbia na hadi sasa tunaendelea kumtafuta, ingawa taarifa zisizo rasmi amekuwa akikimbilia Kongo,”amesema Jenerali Mbungo
Aidha, Mhasibu huyo anatuhumiwa kujipatia mali nyingi na inadaiwa anamiliki maghorofa, magari, pikipiki, nyumba za kawaida na za kifahari na kawaida na viwanda katika mikoa mbalimbali.
-
Lukuvi aagiza kukamatwa kwa maafisa ardhi
-
Takukuru yaanza kulifanyia kazi agizo la Dkt. Kigwangalla
-
TRA yaongeza ufanisi ukusanyaji kodi ya majengo
Hata hivyo, mtumishi huyo anadaiwa kumiliki viwanja, Bunju, Kigamboni, Buyuni (Dar es salaam), Bagamoyo, Kibaha(Pwani), Kihonda, Kihegea, Lukobe (Morogoro), Kisasa, Itege, Chidachi (Dodoma) na Zuguni, Nyegezi, Nyamuhongolo, Nyamagana, Bugarika (Mwanza), viwanja vingine viko Makoko(Musoma), Gomba (Arusha) Mwambani na Mwakidila(Tanga) huku pia anamiliki magari matano ya kifahari na pikipiki