Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) imetenga kiasi cha shilingi milioni 10 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa aliyekuwa mhasibu wa Taasisi hiyo, Godfrey Gugai.

Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Bregadia Jenerali, John Mbungo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa mtumishi huyo awali alionyesha ushirikiano wa kujibu tuhuma zilizokuwa zikimkabili lakini ghafla alitoweka.

“Alielekea  kuonyesha ushirikiano lakini alipoona  hana maelezo ya namna gani alizipata hizo mali akaamua kukimbia na hadi sasa tunaendelea kumtafuta, ingawa taarifa zisizo rasmi amekuwa akikimbilia Kongo,”amesema  Jenerali Mbungo

Aidha, Mhasibu huyo anatuhumiwa kujipatia mali nyingi na inadaiwa anamiliki maghorofa, magari, pikipiki, nyumba za kawaida na za kifahari na kawaida na viwanda katika mikoa mbalimbali.

Hata hivyo, mtumishi huyo anadaiwa kumiliki viwanja, Bunju, Kigamboni, Buyuni (Dar es salaam), Bagamoyo, Kibaha(Pwani), Kihonda, Kihegea, Lukobe (Morogoro), Kisasa, Itege, Chidachi (Dodoma) na Zuguni, Nyegezi, Nyamuhongolo, Nyamagana, Bugarika (Mwanza), viwanja vingine viko Makoko(Musoma), Gomba (Arusha) Mwambani na Mwakidila(Tanga) huku pia anamiliki magari matano ya kifahari na pikipiki

Masha awaweka njiapanda Chadema
Makala: Kwanini unahitaji mazoezi kudhibiti mwili? Ni tatizo la Dunia…