Changamoto ya Uchakavu wa Miundombinu pamoja na Upungufu wa Vyumba vya Madarasa katika shule za Msingi na Sekondari Halmashauri ya wilaya ya Mtwara huenda ikapungua katika kipindi cha muda mfupi kuanzia sasa baada ya Serikali kupeleka zaidi ya Shingi Milion 451 kwa ajili ya kujenga Mabweni na Vyumba vya Madarasa.
Hayo yamesema na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Omary Kipanga wakati akitoa taarifa katika kikao cha kawaida cha baraza la Madiwani ambapo amesema kuwa tayari kiasi hicho cha fedha kimesha ingizwa kwenye Akaunti za Shule husika tayari kuanza kutumika.
Amesema kuwa fedha hizo zimeelekezwa katika sekta ya Elimu Kwa shule za Msingi na Sekondari, ambapo kwa upande wa Sekondari zitajenga, Mabweni makubwa na ya kisasa pamoja na vyumba vya Madarasa kwa shule mbili za Sekondari Kisiwa na Libobe huku upande wa Elimu ya Msingi zitatumika kujenga vyumba vya Madarasa katika shule tatu ambazo ni Mitambo, Dihimba na Mangopachanne.
“Shule ya Sekondari Kisiwa imetengewa kiasi cha shilingi Milioni 190 ambayo pale kutajengwa Mabweni Mawili wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kwa kila Bweni moja ambapo jumla tutakua na wanafunzi 160 pamoja na Vyumba viwili vya Madarasa, na Shule nyingine ni Sekondari MLibobe hii imetengewea kiasi cha Shilingi Milioni 115 na kutajengwa Bweni Moja la wanafunzi 80 pamoja na Vyumba viwili vya Madarasa,” Amesema Kipanga.
Kwa upane wake, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Dkt. Gilly Maleko amewataka madiwani hao kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wananchi katika kujitolea nguvu kazi kwakua fedha hizo zimeelekezwa katika ujenzi wa Vyumba vya Madarasa na Mabweni pekee lakini bado kuna uhitaji mkubwa wa Matundu ya Vyoo jukumu ambalo linaweza kutekelezwa na wazazi, kauli ambayo pia iliungwa mkono na mkuu wa wilaya hiyo ya Mtwara Evod Mmanda
-
Mkuchika awaangukia Ma RC, DC, ‘Msiniponze jamani’
-
Mlinga amuomba JPM ashtukie mtego wa Chadema, amgusa Masoud Kipanya
-
Watumishi 50 wilaya ya Makete kusimamishwa kazi
Hata hiyo, kukamilika kwa miradi hiyo kutapunguza msongamano wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari uliotokana na ongezeko la ufaulu ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Mtwara unakumbukumbu ya kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba mwaka jana