Mahujaji milioni moja kutoka ulimwenguni kote, wamekusanyika katika mji mtakatifu wa Saudi Arabia wa Mecca, kutekeleza ibada kuu ya kwanza ya hija ya Kiislamu tangu kuanza kwa janga la Uviko-19.

Mahujaji hao, wametumia siku kadhaa kutekeleza mfululizo wa mila zinazokusudiwa kuwaleta karibu na Mwenyezi Mungu, wakitembea katika njia iliyopitiwa na Mtume Muhammad takriban miaka 1,400 iliyopita.

Hatua hiyo inajumuisha kusali kwa kuzunguka Kaaba yenye umbo la mchemraba, kaburi takatifu zaidi katika Uislamu, katikati ya ua wa wazi wa Msikiti Mkuu Julai 6, 2022 ambapo maelfu ya mahujaji walishiriki.

Katika kufanikisha ibada hiyo, Waislam mahujaji walisogea kinyume cha saa mara saba kuzunguka jengo la granite, mioyo yao ikiinama kuelekea kwenye muundo uliokusudiwa kuashiria umoja wa Mungu katika Uislamu.

Mwaka huu, hajj iko wazi kwa mahujaji milioni moja wa kigeni na wa ndani, ambao wamepata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19,waliothibitishwa kuwa hawana ugonjwa huo na wako kati ya umri wa miaka 18 hadi 65.

Ingawa, idadi ya mahujaji kwa mwaka huu iko chini ikilinganishwa na ile ya awali kabla ya janga la Uviko-19 la mahujaji milioni 2.5, bado inaashiria kiu ya waislam katika kutimiza azma yao ya Hijja.

UN ‘yakuna kichwa’ idadi ya waathiriwa baa la njaa
Tanzania, Afrika Kusini zasaini makubaliano ya Elimu Kiswahili