Jeshi la Polisi limefanikiwa kuvunja mtandao wa uhalifu wa kundi la Malonjo, baada ya kuwakamata watu saba akiwemo Kiongozi wa wao Juma Hamza maarufu kama Jambazi (27), ambao kwa pamoja walikuwa wanatuhumiwa kwa ubakaji, wizi na unyang’anyi wa kutumia silaha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo Februari 10, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, George Katabazi amesema watu hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 20-30 pia walikuwa wakituhumkwa kuwajeruhi na kuwapora watu vitu mbalimbali.
Amesema, “Juma Hamza maarufu jambazi 27 na wenzake sita (miaka 20-30) wanashikiliwa kwa tuhuma za kuwajeruhi watu watatu, ni mtandao wa wahalifu wakijulikana kwa jina la Malonjoo wakijihusisha na uhalifu mbalimbali.”
Katika tukio la pili, Kamanda Katabazi amesema Polisi inamshikilia Mtu mmoja Omary Bakari kwa tuhuma za kusafirisha kilo 148 za Dawa za kulevya aina ya Mirungu kinyume chasheria.
Bakari anadaiwa kusafirisha Mirungi hiyo kwa kutumia Gari aina ya Mistubishi Kenta yenye namba za usajili T 220 ABF ambalo lilikuwa na chumba maalumu cha kuhifadhi dawa hizo, ili isiwezi gugundulika na mtuhumiwa asiweze kukamatwa.