Wilayani Rufiji, idadi ya wanafuzni wanaokatisha masomo yao kwa sababu ya kugunduliwa na  mimba yazidi kuongezeka, ambapo Mkuu wa wilaya, Juma Njwayo ametoa takimwi za wasichana  wa shule ya sekondari  na msingi zikionesha  wamebainika kuwa wana mimba.
 
Juma Njwayo amesema kuwa mpaka sasa wanafunzi 8 wa Sekondari wametiwa mimba huku wanafunzi wengine saba wakitokea shule ya msingi wamebainka kuwa na mimba.
 

Mkuu huyo wa Wilaya amezungumza na wazazi na walezi na kusema kuwa mimba za utotoni zinakwamsha jitihada za kumkomboa mtoto wa kike kitaaluma, na kusisitiza kuwa elimu ni muhimu, ni nguzo na msingi wa maisha ya mzazi na mtoto wake pia.

”kati ya mimba zilizobainika mwanafunzi mmoja ni wa shule ya sekondari Ngorongo ,Nambunju saba na wengine saba ni wa shule za msingi”, amesema mkuu wa Wilaya 
 
Hivyo ametoa ufafanuzi wa kisheria nakutaja hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kwa wahusika wanaotia mimba za utotoni, hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa wanatengeneza mazingira mazuri shuleni ili kuwaelimisha watoto kujiepusha na udanganyifu.
 
Hayo ameyazungumza katika ziara yake ya mwezi mmoja ya kutembelea shule 43 baada ya kupata taarifa kuwa kuna wanafunzi watoro wa kudumu 190 kati ya wanafunzi 2,442 wanaotarajiwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu .
 
Aidha katika ziara hiyo amefanikiwa kuwarejesha shule wanafunzi hao 54 wa shule ya Ikwiriri ,shule ya msingi Utete tisa na shule ya msingi Mapinduzi tisa na kukazia kuwepo uhusiano mzuri kati ya mzazi  na mwalimu, pia amewaasa wazazi kujenga utamaduni wa kuwafuatilia watoto wao.

Video: Rick Ross aachia ngoma mpya ya 'Lamborghini doors' yumo Meek Mill
Harry Kane amaliza ukame wa mabao Uingereza ikishinda dhidi ya Malta