Aliyekuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Mbeya City Fc, Meja mstaafu Abdul Mingange, ametangazwa rasmi kuwa kocha mkuu kuchukua nafasi ya Juma Mwambusi aliyejiunga na Yanga miezi miwili iliyopita.

Akizungumza mara baada ya kumkabidhi barua rasmi ya kupewa nafasi hiyo,Mwenyekiti wa City, Musa Mapunda, alisema kuwa uongozi wa Halmashauri ya jiji na bodi ya timu kwa ujumla wameridhishwa na utendaji kazi wa kocha Mingange hivyo kwa pamoja kuamua kumkabidhi jukumu la kuwa kocha mkuu kufuatia kazi nzuri aliyoifanya akiwa msiadizi wa kocha Mwambusi kabla na baada ya kuondoka kwake.

“Tumeridhishwa na utendaji kazi wake mzuri, amekuwa na msaada mkubwa kabla na baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha wetu mkuu,ni mwalimu wa daraja la juu, tuna imani kubwa juu yake na hakika ataisadia timu yetu katika kutafuta mafanikio zaidi ya yaliyokuwepo” alisema Mwenyekiti.

Kwa upande wake kocha Mingange mara baaada ya kukabidhiwa barua ya kuthitishiwa nafasi hiyo alisema amefurahishwa na hatua na uongozi kumuamini na kumpa jukumu hilo kilichobaki kwake ni kufanya kazi ili kufanikisha malengo ya timu na uongozi katika kuipa mafanaikio City.

“Nina furaha, hili ni jambo kubwa kwangu, naushukuru uongozi kwa kuniamini na kunipa jukumu hili, City ni timu kubwa, imekuwa na mafanikio katika misimu yote tangu ilipopanda daraja,kilichobaki kwangu ni kufanya kazi ili kutimiza malengo yote yaliyopo, sina wasiwasi na hili kwa sababu napata ushirikiano mzuri kutoka pande zote kwa maana ya viongozi na wachezaji, ninachoweza kusema huu ni msimu mwingine timu yangu inakwenda kuandika historia mpya” alisema.

Kocha Mingange amekabidiwa barua hiyo rasmi ya kuwa kocha mkuu kwenye kambi ya muda ya City iliyopo chuo cha ualimu wilayani Rungwe, jijini Mbeya mbele ya wachezaji wote wa City.

TAARIFA NI KWA MUJIBU WA TOVUTI YA KLABU YA MBEYA CITY

Point Tatu Za EPL Kusakwa Weekend Hii
Wajumbe Wa Bodi Ya Ligi Kukutana