Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ndanda FC na kikosi cha vijana cha Azam FC chini ya umri wa miaka 20 Abdul  Mingange, amezitahadharisha klabu za soka nchini, dhidi ya Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC.

Mingange ambaye pia aliwahi kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC, amesema klabu za soka nchini zinapaswa kucheza kwa heshima kubwa dhidi ya Simba SC, pindi wanapokuatana nayo kwenye michuano ya Ligi Kuu ama Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Tahadhari ya kocha huyo mzawa imekuja, baada ya kuishuhudia klabu yake ya zamani Mbeya City ikikubali kufungwa mabao manne kwa moja, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara jana Jumanne (Juni 22), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

“Nimezungumza Mara nyingi na wanaonielewa wananielewa. Simba wana kikosi kimekaa pamoja, wachezaji wake zaidi ya 70% wamepata challenge nyingi na kubwa kubwa kuliko hizi timu zetu za ligi yetu. Huwa nasema team strategy na team formation huwa haina maana Kama hakuna players functions fully.”

“Tatizo la walimu wengi wanapotaka kucheza na Simba wanataka wapate matokeo. Kuna instructor wangu mzoefu duniani katika kufundisha soka alinieleza hivi. Kwanza unapasa kufahamu nguvu ya mpinzani wako, na mapungufu yao. Pili fahamu ni wachezaji gani hatari wakiwa kwenye maeneo hatarishi kwako. Jambo lingine jipime uwezo wa timu yako na nguvu ulizonazo utazitumiaje.”

“Ukicheza na Simba Kuna wachezaji 4 ndiyo hatari Sana wanapokuwa na mpira wakiwa kwenye nusu yako. Siwataji kwa sababu za kiusalama kimpira. Pili wachezaji wako wasiwe wavivu. Timu inayo kaa na mpira muda wote akitokea mvivu upande wenu mjue mashimo yatakuwa mengi. Tatu wachezaji wengi watanzania ni ball watcher.”

“Wanachelewa kuona na kufikiri( tactical perception). Tatu wachezaji wetu hawajui kipi hatari uwanjani wanadhani mpira ni hatari. Kwanza space ndiyo hatari, mbili opponent, tatu ndiyo mpira.”

“Huwa naangalia Sana wachezaji wengi watanzania wanamatatizo hayo. Tatizo wamekosa kufundishwa mpira wa maarifa mapema. Walioangalia mpira wa Yanga vs Mwadui, Mchezaji aliyefunga kwa kichwa, aliruka nyuma ya Dickson Job, free header kwa sababu Job hajamuona striker kuwa yupo nyuma yake. Tatizo lingine wachezaji wetu wanakosa spartial awareness.”

“Fitness Kuna maeneo yanatakiwa yajengwe zaidi kuliko maeneo mengine. Ndiyo maana mpira wa Sasa unahitaji wataalamu wengi si kocha mkuu tu. Fitness trainer, goalkeeping coach , psychologist, nk.” Amesema Kocha huyoa mbaye ni Meja Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Serikali yajipanga kukomesha ukatili wa kijinsia katika vyombo vya habari
ASFC: Nyoni kutoa tiketi 50