Baada ya Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano ya Viwanda nchini Uganda, Kanali mstaafu Charles Okello Engola kuuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake ambaye pia dakika chache baadaye alijiua kwa kujipiga risasi taarifa zimeibuka kuwa Mlinzi huyo alikuwa ikidaiwa kuwa alikuwa akilalamikia kutolipwa mshahara kwa muda mrefu.

Mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo, alisema mlinzi huyo alikuwa akilalamikia kutolipwa mshahara wake kitendo ambacho kilisababisha kuchukua maamuzi hayo ingawa hakuweza kuthibitisha madeai hayo kiufasaha.

Mlinzi yule hakuwa amelipwa, alisema ana mke ambaye ni mjamzito na watoto wake hawakuwa wanaenda shuleni wakati wa muajiri wake watoto wake walikuwa wanaenda shule, alisema shuhuda huyo wa mauaji ya Waziri Engola ambaye aliwahi pia kuhudumu pia kama Naibu waziri wa Ulinzi.

Kanali mstaafu Charles Okello Engola.

Kanali Engola aliuawa nyumbani kwake Kyanja jijini Kampala, na mlinzi wake huku baadhi ya walioshuhudia tukio hilo wakisema, mlinzi huyo alizunguka katika eneo hilo akifyatua risasi hewani mara baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Baadaye Naibu msemaji wa polisi wa Kampala Metropolitan, Luke Owoyesigire alithibitisha kutokea kwa tukio hilo sambamba na Spika wa bunge la Uganda, Anita Among ambaye naye mbele ya Bunge akithibitisha tukio la kifo cha Charles Okello Engola.

Muda mfupi baadaye Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akaipiga simu kwa familia ya Waziri huyo, ili kuwafariji na kwa mujibu wa Waziri wa Habari na ICT, Chris Baryomunsi alisema Rais Museveni alitaka kujua mazingira ambayo waziri huyo aliuawa wakati alipokuwa akitoka kuelekea kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri.

Naibu Spika wa Bunge la Uganda, Thomas Tayebwa yeye akawa ni miongoni mwa Viongozi wa ngazi za juu Serikali waliotembelea nyumbani kwa waziri huyo muda mfupi baada ya kuuawa huku Mshauri Mkuu wa Rais kuhusu operesheni maalum Jenerali Muhoozi Kainerugaba (Mtoto wa Rais Museveni), aliandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa, “Inasikitisha sana kusikia kuhusu kifo cha kusikitisha cha Kanali (mst) Charles Engola, ni hasara ya kutisha kwa nchi. Roho yake ipumzike kwa amani ya milele.”

Wengi wakajitokeza kuhani msiba huo akiwemo pia Kiongozi wa Jukwaa la Umoja wa Kitaifa wa Upinzani, Robert Kyagulanyi (Bobi Wine), ambaye yeye alisema “Uganda hakuna aliye salama. Hata wale tunaotarajia waidumishe wanaiondoa. Pumzika kwa amani Kanali Mstaafu Charles Okello Engola. Pole kwa familia na wananchi wa Kitongoji cha Lango.

Meridianbet inakujali mteja mpya
Mpole hali tete DR Congo, kurudi Tanzania