Kocha Mkuu wa Maafande wa Magereza ‘Tanzania Prisons’, Fred Felix Minziro amewataka mashabiki wa timu hiyo na wakazi wa Jiji la Mbeya kwenda kuushuhudia ushindi wa kwanza kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Simba SC.

Minziro ameyaeleza hayo baada ya kukamilisha maandalizi ya mchezo huo wa kwanza msimu huu utakaopigwa Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya kesho Alhamisi (Oktoba 05).

Prisons ina yoburuza mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa pointi moja, imecheza mechi tatu ugenini mpaka sasa ambapo imetoa sare mechi moja na kufungwa mara mbili.

“Maandalizi yamekwenda vizuri, tumejaribu kufanya masahihisho ya hapa na pale kutokana na mechi zilizopita.

“Siwezi kusema naahidi nini lakini tunakutana na mchezo mgumu ila mashabiki wa Prisons na wananchi wa Mbeya waje kwa wingi kusapoti kuhakikisha tunapata matokeo kwenye mechi yetu ya kwanza hapa nyumbani,” amesema Minziro.

Wakati hali ikiwa hivyo Prisons, Simba yenyewe imeshinda michezo yake mitatu ya ligi ya awali ikiwa inashika nafasi ya pili kwa pointi tisa, sawa na vinara Young Africans ambao wako juu kwa idadi ya mabao ya kufunga.

Tayari kikosi cha Simba SC kimeshawasili jijini MBeya tangu jana usiku, kwa ajili ya mchezo huo utakaoanza mishale ya saa kumi jioni.

Pochettino aanza kumfikiria Marc Cucurella
Arsenal wamuita mezani Ben White