Katika wiki iliyokuwa na pilikapilika ni hii hapa ambayo imeisha jana. Kama utakumbuka jumatano ya wiki hii Kulikuwa na Sikukuu ya Eid Ul Fitr huku alhamisi ikiwa ni siku ya wafanyabiashara yaani saba saba na ijumaa ikawa inaunganisha  wikiend (mwisho wa wiki)

Na katika wikiend hii mastaa kibao walioneshana ubabe katika ulimwengu wa urembo na mitindo ‘fashion’ kutokana na matukio tofauti tofauti ambayo walikutana.

Kutana na baadhi ya mastaa ambao wao walitendea haki mavazi yao katika shughuli ambazo walikuwepo mwishoni mwa wiki hii. Picha hizi hazipo katika mtiririko maalumu .

linnas

Mwanamuziki Linnah Sanga katika black tie iliyoandaliwa na wema sepetu pamoja Muna Logistics hakuacha kuonesha ubabe wake katika urembo na mitindo

uwyaa

Muigizaji maarufu Irine Uwoya naye wikiend yake haikua haba katika ulimwengu wa fashion na katika Black tie huu ulikua muonekano wake.

dem

Muimbaji wa kizazi kipya Ben Pol akiwa na Hamisa Mobeto katika usiku wa RnB na moyo mashine Special night maisha basement walinoga kutokana na shughuli maalum.

hamisa

Mwanamitindo na Muigizaji,Hamisa Mobeto pamoja na dada wa Diamond Platnumz, Esma Platnumz  kwenye usiku wa birthday party ya Mama Diamond

mama chibu

Mama mzazi wa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Bi Sandra naye ulimwengu wa fashion haujamuacha kutokana na umri wake na hivi ndivyo alivyoonekana katika usiku wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

sultan

Wema Sepetu pamoja na anayetajwa kuwa ni mpenzi wake wa sasa Idris Sultani nao hawakuacha kutoa heshima  katika ulimwengu wa urembo na mitindo kwenye usiku wa black tie.

Hata hivyo wafuatiliaji wengi wa mambo haya hawakuacha kuonesha kufurahishwa na mionekano ya mama Diamond pamoja na Wema Sepetu kuwa kwa wiki hii walikuwa wababe katika ulimwengu wa urembo na Mitindo.

 

 

mobeto

 

 

 

Video: Highlights za Finali na Matukio Yaliyovutia EURO 2016
Zeben Hernandez: Azam FC Mpya Inakuja