Waziri wa Fedha na Mpango Philip Mpango, amewataka wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma ambao wamechangia mfuko mkuu wa Serikali chini ya kiwango kujieleza ndani ya siku 9 kuanzia Desemba 22.
Mpango ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma alipokutana na wakuu wa Taasisi za Serikali na Mashariki ya Umma 236.
Wakuu wa Taasisi na Mashirika wametakiwa kujieleza kuhusu kutokuchangia huduma za jamii pamoja na kutokuzingatia ukomo wa matumizi ya asilimia 60 ya mapato ghafi ya Taasisi kwa mujibu wa sheria ya fedha.
Aidha Waziri Mpango amezitaka taasisi hizo kuhakikisha wanapunguza matumizi yasiyo ya lazima ikiwemo misafara mikubwa ya watendaji na wajumbe wa Bodi kutembelea miradi.