Klabu za Arsenal na Chelsea zimezidi kupoteza matumaini ya kutaka kumsajili Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka nchini Italia SSC Napoli, Victor Osimhen baada ya Rais wa klabu hiyo, Aurelio De Laurentiis kuweka wazi fundi huyo yupo kwenye hatua za mwisho kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye kikosi chao.

Timu zote hizi zimekuwa zikihusishwa kutaka kumsajli Osimhen dirisha lijalo, lakini kama ataongezwa mkataba mpya itakuwa ngumu kwa sababu SSC Napoli itahitaji kiasi kikubwa zaidi cha pesa.

Mbali ya Arsenal na Chelsea, timu nyingi barani Ulaya zilihitaji kutaka kumsajili fundi huyu wa kimataifa wa Nigeria ambaye amekuwa na kiwango bora tangu msimu uliopita.

Osimhen pia alihitajika na baadhi yatimu kutoka Saudia lakini ilishindikana baada ya Osimhen mwenyewe kukataa na kusisitiza mipango yake ni kuendelea kucheza soka la kiushindani barani Ulaya.

Mkataba wa sasa wa fundi huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

Nyara za Serikali, unyang'anyi: 121 wafikishwa Mahakamani
Xavi: Ninampenda sana Alvaro Morata