Kama ambavyo tujuavyo ya kwamba mafanikio ni matokeo yatokanayo na mipango ambayo mtu amejipangia na kuitekeleza mipango hiyo yeye mwenyewe.
Ukweli ambao upo bayana ni kwamba mipango mingi hufa katika hatua za awali kabisa yaani mtu anapowaza tu anajikuta umeingiwa na roho ya kushindwa roho ya kutokujiamini kuwa kupitia wazo lake anaweza kufanya kitu au anaweza kubadilisha kitu katika maisha yake, watu wengi wamefungwa na roho za uoga na roho za kutokujiamini.
Kwa siku mwanadamu huwaza mawazo mengi sana yale ambayo ni hasi na chanya pia, lakini changomoto kubwa huja katika namna ambavyo mtu atanavyoamua kuchukua hatua stahiki juu ya mawazo chanya anayowaza kila wakati.
Wengi tunawaza vizuri sana lakini mawazo hayo hufa pasipo kwenda katika hatua ya utekelezaji, wengi wetu tumejikuta tukighairisha kufanya mambo ya msingi kwa sababu tumekuwa ni wavivu wa kuchambua mawazo yetu ya msingi kwa kina zaidi.
Unakuta mtu ana wazo fulani la msingi lakini changamoto inakuja katika kugeuza mawazo hayo kuwa kitu halisi,
Hivyo kama una kiu ya kupiga hatua za mafaniko, unatakiwa kukumbuka mipango mingi ya kimafanikio hufa mapema sana kama mtu huyo hatakuwa makini katika kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa.
kila wakati ikumbukwe ili kuweza kufanikiwa kimaisha unatakiwa kukumbuka ya kwamba kila kitu tunachokiwaza tunatakiwa kuchukua hatua stahiki juu ya kitu hicho na si kuishia kuwaza tu.