Kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili wa Nusu Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaopigwa keshokutwa Jumatano (Mei 17) dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Kocha Mkuu wa Young Africans, Nasreddine Nabi amemaliza hesabu baada ya kuwaandaa nyota wake watano kwa ajili ya kuumaliza mchezo huo.

Young Africans itakuwa mgeni wa mchezo huo utakaochezwa mjini Rustenburg katika Uwanja wa Royal Bafokeng majira ya saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Mipango ya Kocha Nabi iko hivi, Young Africans juzi Jumamosi (Mei 13) ilicheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar ambapo Young Africans waliibuka na ushindi wa mabao 4-2 na kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

Katika mchezo huo Nabi aliwapumzisha wachezaji watano ambao walianza katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Marumo iliyopigwa Dar ambayo Young Africans waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Wachezaji ambao walianza kwenye nusu hiyo ambao hawakuwa sehemu ya mchezo wa juzi Jumamosi (Mei 13) dhidi ya Dodoma ni Djigui Diarra, Khalid Aucho, Dickson Job, Ibrahim Bacca na nahodha Bakari Mwamnyeto.

Nabi amesema: “Tumekuwa na ratiba ya michezo mingi migumu ambayo imefuatana, hivyo ili kupunguza majeraha na kuhakikisha tunakuwa na wachezaji ambao wana utimamu sahihi wa miili tulilazimika mabadiliko hayo ya kufanya lazima.”

Meridianbet Kasino Jackpot ya Kibabe
Klopp: Nunez angefikisha mabao 20 msimu huu