Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliviera Robertinho ametoa onyo zito kwa wachezaji wake wakati wakijiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Simba SC hivi sasa ipo katika maandalizi ya mchezo wao hatua ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakaocheza dhidi ya Mabingwa wa Zambia Power Dynamos.
Simba SC tofauti na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, pia ipo katika maandalizi African Football League itakayoanza Oktoba 20 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ikitarajia kupapatuana na Al Ahly ya Misri.
Robertinho amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakibweteka wanapopata ushindi kiduchu katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu Bara, jambo ambalo hatakia kuliona likijitokeza tena kikosini kwake.
Robertinho amesema kuwa hataki kuwaona wachezaji hao, wakibweteka katika kuelekea michezo ijayo ya msimu huu ikiwemo ya ile kimataifa ambayo ni itawakutanisha na timu ya Zambia na kisha Misri
Ameongeza kuwa kikubwa anataka kuona timu yake ikipata ushindi mkubwa wa mabao ambayo mbeleni yatakuwa na faida kubwa kwao.
Ninaamini uwezo na ubora mkubwa ambao wanao wachezaji wangu kama sehemu ya katika kikosi changu cha msimu huu, kama wakicheza kwa kujituma, basi tutafikia malengo.
“Hivyo nimewaonya wachezaji wangu kwa kuwataka kuongeza umakini kwa kufunga mabao mengi katika kila nafasi tutakayoipata uwanjani.
“Hilo ni jukumu la kila mchezaji kufunga na kutengeneza mabao wakati tukijiandaa na michuano ya kimataifa ambayo ni migumu, mbeleni idadi kubwa ya mabao itatusadia itakapohitajika,” amesema Robertinho.