Wakati mazoezi ya kikosi cha Simba SC kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya makundi dhidi ya AS Vita yakizidi kupamba moto, wachezaji wawili wa mabingwa hao wa Tanzania, Luis Miquissone na Meddie Kagere ndio wanaochelewesha mipango ya miamba hiyo ya soka nchini, imeelezwa.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, amesema wachezaji wote waliokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wameungana na wenzao huku baadhi yao walikuwapo katika mataifa yao walitarajiwa kuungana na wenzao jana isipokuwa Miquissone na Kagere.

Amesema Miquissone na Kagere wao wataripoti kambini leo Alhamisi kwa sababu timu zao za taifa zilikuwa na michezo siku ya Jumanne (Machi 30).

Katika mchezo huo, Simba SC itakuwa ikihitaji sare tu ili kufuzu hatua ya robo fainali, wakati AS Vita yenyewe ikihitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi ya kufuzu hatua hiyo, wakati huu Al Ahly ambao watakuwa ugenini dhidi ya vibonde wa kundi hilo, Al-Merrikh ya Sudan yenye alama moja, nayo ikihitaji ushindi huku ikiombea Wekundu wa Msimbazi hao washinde ili nao wakate tiketi kabla ya mchezo wa mwisho.

Namungo FC: Jumapili tuna jambo letu
Mashabiki 10,000 kushuhudia Simba Vs AS Vita