Kiungo kutoka nchini Bosnia na Herzegovina Miralem Pjanic, anajiandaa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa wa soka Italia Juventus FC.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, anatarajiwa kukamilisha mpango huo baadae (leo Alkhamis), na mkataba wake mpya utamuwezesha kulipwa mshahara wa Euro milioni 7 kwa mwaka hadi mwezi Juni mwaka 2022.
Mkataba wa awali ulikua unamuwezesha kulipwa mshara wa Euro milioni 4.5 kwa mwaka sawa na ilivyo kwa mshambuliaji kutoka nchini Argentina Paulo Dybala.
Mkataba wa sasa wa Pjanic umesaliwa na mwaka mmoja, na uongozi wa Juventus umeona kuna ulazima kumsainisha mkataba mpya ili kuhofia asije akaondoka kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu wa 2018/19.
Tayari klabu kama FC Barcelona, Paris Saint-Germain na Real Madrid zilikua zinatajwa kumuwania kiungo huyo, ambaye mpaka sasa ameshaitumikia Juventus katika michezo 61 na kufunga mabao 10.
Pjanic alijiungana Juventus FC mwaka 2016 akitokea kwa wababe wa Stadio Olimpico AS Roma, kwa ada ya Euro milioni 32.