MISRI imejitoa kwenye Michezo ya Afrika kwa timu zote za wanaume na wanawake ambayo itafanyika mjini Brazzaville, Kongo mwaka 2015.

Kwa mujibu wa ibara ya 19 (B) ya kanuni za mashindano hayo isemayo; “Ikiwa timu itajitoa baada ya kufuzu kwenye fainali za michuano kabla ya kuanza, Kamati ya Maandalizi itazichukua timu zilizotolewa na timu zilizofuzu kuingia kwenye fainali kama mazingira yanaruhusu,”.

Timu mbili zilizotolewa na Misri katika mechi za kufuzu ni Senegal kwa wanawake na Burundi kwa wanaume ambazo sasa zinaweza kupewa nafasi hiyo.

Upande wa wanawake timu zilizofuzu mbali ya Misri ni wenyeji Kongo, Nigeria, Tanzania na Ivory Coast zilizopangwa Kundi A wakati Kundi B kuna Cameroon, Ghana na Afrika Kusini.

Kwa wanaume mbali na Misri Kundi A kuna wenyeji Kongo, Sudan, Zimbabwe na Burkina Faso wakati Kundi B kuna Ghana, Senegal na Nigeria na michuano hiyo inatarajiwa kuanza Septemba 6 hadi 18 mwaka huu mjini Brazzaville, Kongo.

Magufuli Aahidi Walimu Maisha Bora Kama ‘Mapadri’
Msenegal Mpya Wa Simba Ashuka Dar es salaam