Warembo wa ‘Miss Ilala 2018’ wamemtembelea mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ofisini kwake Ilala kwa ajili ya kumpongeza na kumshukuru kama mlezi wa wilaya ya Ilala na kuomba baraka kwa ajili ya mashindano ya Miss Dar es Salam 2018.
Warembo hao walioingia tano bora ambao wamepata tiketi ya kushiriki mashindano ya ngazi ya mkoa waliongozana na Kamati ya Miss Ilala ambao ndio waliandaa mashindano hayo mwaka huu.
Akizungumza, Miss Ilala 2018, Linda Samson amempongeza Mkuu wa wilaya kwa kuwasimamia washindi wote kupata zawadi.
“Tunashukuru mashindano yetu ngazi ya wilaya yamemalizika kwa sasa tunakwenda kupeperusha Bendera ngazi ya mkoa, ” amesema Linda.
Linda amesema wanakwenda kupeperusha Bendera ya Ilala ngazi, ya mkoa na baadaye Miss Tanzania, hivyo wamemwahidi DC Mjema kuwa watafanya vizuri na kuibuka Miss Tanzania mwaka huu .
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewapongeza warembo hao watano ambao wamefanikiwa kushiriki Miss Dar es salaam, ambapo amewapa baraka zake na kuwapa moyo huko wanapokwenda wakafanye vizuri zaidi.
“Warembo wa wilaya ya yangu msiwe na hofu naomba mjiamini mashindano ambayo mnakwenda kushiriki naamini mtafanya vizuri kwa wilaya yangu ” amesema Mjema.
Naye Mratibu wa Miss Ilala, Lucas Lutainrwa amesema mashindano ya Miss Ilala mwaka huu 20018 yameshirikisha warembo 19 Kati ya warembo watano wamefanikiwa kusonga mbele Miss Dar es salaam.
Aidha, Lucas ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais kwa utendaji wa kazi na utekelezaji wa Ilani vizuri katika Serikali ya awamu ya tano changamoto mbalimbali zimekwisha katika wilaya Ilala sehemu ya mafanikio ya kujivunia wananchi wanapata huduma zote za kijamii .
Lucas ametaja warembo wake 19 mwaka 2018 walishiriki Miss Ilala, ambapo mrembo Linda Samson alifanikiwa kutwaa taji la Ilala mwaka huu, nafasi ya pili Sheila Rajabu,nafasi ya Tatu Husna Jamal nafasi ya nne Magreth Geddy nafasi ya tano Jessa Sophia.