Regina Ndimbo, ni mshiriki wa Miss Kinondoni aliyeshika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro hiko cha kulivaa taji la Miss Kinondoni, baada ya kushindwa kuwa mshindi namba mmoja mshiriki huyo ameamua kujishughulisha na shughuli za kuitumikia jamii.

Kutokana na kampeni inayoendelea Dar es salaam vita dhidi ya madawa ya kulevya, inayosimamiwa rasmi na muheshimiwa Paul Makonda, mkuu wa mkoa huo. Kila kona ya mji watu huzungumzia vita hii kwa namna na mtazamo tofauti.

Mlimbwende huyu amepata nafasi ya kuongelea swala hili  la madawa ya kulevya na kueleza tamaa ya fedha ndio sababu kubwa inayowafanya watu maarufu kwenye tasnia ya burudani kujihusisha na dawa ya kulevya.

”Maisha mazuri bila kuvuja jasho yanawaponza mastaa wengi, mtu akishapata jina hapa mjini kila mtu atakufuata uwe naye karibu kuna wengine wazuri wengine watakuletea michongo ya madawa ya kulevya utajikuta taratibu unaingia kwenye biashara hiyo” amesema Regina.

Ameendelea kwa kusema ustaa unatumika kama mwanya wa kufanikisha biashara hiyo. Watu wazito wanajihusisha na madawa ya kulevya huwatumia wasanii.

”Tuunge mkono jitihada za serikali kupinga madawa ya kulevya, watu wazito kwenye biashara hiyo wamekuja kutuharibia vijana na mbaya zaidi ndiyo nguvu kazi ya Taifa , ngoja tuone serikali itakapoishia kupigana vita” Amesema Regina

 

Ruud Gullit: Vardy, Mahrez Wangeruhusiwa Kuondoka
Gareth Bale Kuwavaa SSC Napoli