Aliyekuwa mshindi wa shindano la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare amekumbwa na kashfa nzito ya ufisadi iliyoiingizia serikali hasara ya shilingi trilioni 1.3.

Shore Sinare alikuwa Afisa mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la Tanzania anadaiwa kuwa miongoni mwa waliohusika na ufisadi huo mwaka 2012 na 2013.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na gazeti la Mwananchi, Sinare anadaiwa kushirikiana na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Stanbic Tanzania, Bashir Awale ambao walifanya ufisadi huo kupitia mauzo ya hati fungani za serikali.

Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Ufisadi ya Uingereza (SFO), iliwasilisha ushahidi wake unaoonesha kwamba kiasi cha shilingi trilioni 1.3 kilipotea wakati wa uuzwaji wa hati fungani za serikali kwa benki ya Stanbic inayomilikiwa na Standard Group ya Afrika Kusini.

Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hosea alimwambia mwandishi wa gazeti hilo kuwa anatambua sakata hilo na kwamba Taasisi hiyo inaendelea kulifanyia kazi.

 

Zitto Kabwe amng'ang'ania Maalim Seif, Awataka ZEC waepushe Shari
Magufuli Aelekeza Matumizi Mapya Fedha Za Sherehe Za Uhuru