Mrembo anayeshikilia tajia la Miss Tanzania 2020 -2021, Rose Manfere, amevuliwa uwakilishi wa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Puerto Rico mwishoni mwa mwaka huu.

Hatua hiyo imechukuliwa na kamati ya Miss Tanzania baada ya kugundua baadhi ya tabia za mrembo huyo ambazo si nzuri na zitakuwa kikwazo cha kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Taarifa kutoka chanzo cha ndani ya Kamati ya Miss Tanzania, zimeeleza kuwa “Mrembo ambaye anatakiwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi anatakiwa awe na tabia njema kuanzia hapa nchi na kufuata kanuni na taratibu za mkataba wake nakwamba akikiuka kamati inatakiwa kuchukua hatua zinazostahili,”

Aidha, chanzo hicho kimesema kuwa, nafasi hiyo amepewa mshindi wa pili wa Miss Tazania 2020-2021 Juliana Rugumisa ambaye kamati imeona ana faa kuwa mwakilishi wa taifa.

Vifo vya fikia 72 Afrika Kusini
Mugalu: Nataka kuwa mfungaji bora Tanzania