Klabu ya Mtibwa Sugar italazimika kusaka ushindi kwa hali na mali katika michezo mitatu ya Ligi Kuu mwezi Mei ambayo itawafanya wavuje jasho ili kufanikisha malengo yao ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mchezo wa kwanza utakuwa dhidi ya Polisi Tanzania iliyo nafasi ya 15 na kwa kufikisha alama 22 unatarajiwa kuchezwa Mei 15, Uwanja wa Ushirika, Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mchezo wake wa tatu dhidi ya Kagera Sugar yenye alama 35 unatarajiwa kupangiwa tarehe huku, mchezo mwingine wa tatu ikiwa ni dhidi ya Geita Gold iliyo na alama 37.
Kwenye michezo hiyo mitatu, miwili itakuwa nyumbani dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold, itakayochezwa Uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro.
Hadi sasa Mtibwa Sugar imekusanya alama 29 ikiwa nafasi ya 12 baada ya kucheza michezo 27.
Charles llanfya, nyota wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wapo tayari kwa na watapambana kupata mechi zilizobaki matokeo.