Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC amesema kuwa hospitali hiyo imezidiwa na wagonjwa wanaohitaji hewa ya Oxgen ambapo amesema kwa siku inatumika mitungi ya gesi zaidi ya 400, ukilinganisha na uzalishaji wake kwa siku ambayo inauwezo wa kuzalisha mitungi 400.
Kwa mujibu a gazeti la Mwananchi Profesa Masenga amesema kuwa Kwa siku mgonjwa mmoja anatumia mitungi 8 hadi 10.
“Kwa siku mgonjwa mmoja anatumia mitungi 8 hadi 10 hili tatizo ni kubwa na wananchi msilichukulie kimzaha mzaha ni ugonjwa hatari sana, tuendelee kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na Wizara ya Afya,” amesema Prof. Masenga.
“Tuna kiwanda hapa KCMC cha kuzalisha mitungi 400 kwa saa 24 na mtambo huu Mungu alitusaidia tukauweka mwaka jana na tuliona hili litatusaidia kwa miaka 20 bila kuwa na shida ya Oksijeni,”amesema Prof. Masenga.
“Matumizi yetu kwa siku yalikuwa ni mitungi 50 hadi 60 lakini ilipofika mwezi wa tatu mwaka jana kwenye wimbi la kwanza la corona tuliona umuhimu wake,”amesema Prof. Masenga
Aidha amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo wa corona na kufuata maelekezo yote yanayoendelea kutolewa na Wizara ya afya.