Haruna Juma, Nsimbo – Katavi.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda ametembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya kuanzishwa programu ya BBT Mifugo Mkoa wa Katavi, lilopo katika Halmashauri ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda.

Akiwa eneo hilo, Pinda amepokea taarifa ya uwekezaji katika eneo hilo kutoka kwa Afisa Mifugo mkoa wa Katavi, Zidiheri Mhando kabla Mkandarasi wa mradi huo, Mhandisi Elimringi Mota hajaelezea maendeleo ya mradi.

Mradi huo uliofikia asilimia 70, unajumuisha ujenzi wa lambo la kunyweshea mifugo litakakuwa na kuhifadhi zaidi ya mita za ujazo 93,000 lililopo kwenye eneo la ukubwa wa zaidi ekari 7,000 huku Pinda akiipongeza Serikali ya Mkoa wa Katavi kwa kuendelea kubuni miradi yenye tija kwa maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kumegwa ekari 12,000 kutoka Hifadhini na kuzirejesha kwa Wananchi.

Hassan Dilunga afunguka kwa uchungu
Mabilioni kuboresha Vituo vya Afya Babati