Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea kipande cha reli cha majaribio na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Isaka – Mwanza katika Stesheni ya Fela mkoani Mwanza.
Majaliwa amefanya ukaguzi huo hii leo Oktoba 16, 2022, na kisha kujionea picha mbalimbali zinazoonyesha miundombinu itakayojengwa katika Reli hiyo akiongozana na viongozi wa Kitaifa, wananchi sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kipande cha reli cha majaribio wakati alipokagua maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR,), Stesheni ya Fela mkoani Mwanza, hii leo Oktoba 16, 2022. akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Amina Lumuli (hawapo pichani).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha mbalimbali zinazoonyesha miundombinu itakayojengwa katika kiapnde cha reli ya kisasa (SGR) cha Mwanza – Isaka wakati alipokagua maendeleo ya Ujenzi wa reli hiyo katika Stesheni ya Fela mkoani Mwanza, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima.
Mara baada ya ukaguzi alioufanya wa kujionea maendeleo ya ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa SGR, Waziri Mkuu pia alipata wasaa wa kuzungumza na Wananchi waliojitokeza katika eneo hilo.