Tetesi zimezuka kuwa rapa Kanye West ‘Ye’ ametoweka kusikojulikana huku mshirika wake wa zamani wa kibiashara akishindwa kumpata ili kumfikisha katika vyombo vya dola kutokana na kesi nzito ya mamilioni ya pesa inaypomkabili.

Nyota huyo wa muziki wa rap na mfanyabiashara maarufu mwenye umri wa miaka 45 anashtakiwa kwa kwa kile kinachodaiwa kuwa anadaiwa kiasi cha pesa kisichopugua $4.5 milioni, ambazo ni sawa na zaidi ya Bilioni 15, na aliyekuwa meneja wa biashara, Thomas St. John, kwa madai ya kutolipwa stahiki zake.

Hata hivyo, Bw St John ameshindwa kumpata Kanye na hata kupata anwani sahihi ya anapopatika nyota huyo kwa sasa, na hivyo inasemekana ameiambia mahakama ya Marekani kwamba anaamini nyota huyo hayupo na kwamba pengine ametoweka kusikojulikana.

ZILIPOANZIA KUENEA TAARIFA ZA KANYE KUTOWEKA

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, uvumi ulienea kwamba Kanye hayupo baada ya tweet iliyotumwa na Daily Loud kusema: “Kanye West ameripotiwa kutoweka na hakuweza kupatikana kwa wiki kadhaa”

Ripoti ya kutoweka kwa Kanye imeelezea jitihada za kumtafuta zilihusisha anwani tatu tofauti huko Los Angeles katika jaribio la kumtafuta Kanye na timu yake, lakini zoezi hilo halikufaulu.

Aidha pamoja na uvumi huo kuenea kwa kasi, upande wa pili baadhi ya mashabiki wameshiriki kwenye mitandaoya kijamii taarifa ya kuwa Kanye West alionekana akihudhuria kanisani huko Los Angeles mnamo Desemba 14, akiwa ameficha baadhi ya sehemu za sura yake huku akiwa amevalia koti la kijani na kofia.

Kanye West kwenye picha ya pamoja na Kim Kardashian pamoja na watoto wao enzi za ndoa yao

Pamoja na hayo, aliyekuwa mke wake Kanye West, mwanamitindo maarufu duniani, Kim Kardashian wiki hii aliangua kilio alipokuwa katika mahojiano maalum na podcast ya Angie Martinez IRL alipokuwa akielezea jinsi wanavyolea watoto wao wanne huku akibainisha madhila anayoendelea kuyapitia kutoka kwa Kanye huku akiweka wazi kuwa vitendo vya Kanye dhidi yake pengine vikaathiri vibaya mahusiano yake yajayo kwenye maisha yake.

“Ni ngumu kuwa mzazi mwenza wa Kanye, ni ngumu” alisema Kim.

Kim na Kanye kwa pamoja walifanikiwa kupata watoto wanne ambao binti yao wa kwanza North, mwenye umri wa miaka tisa, na Chicago, wanne, na wana Saint, saba, na Zaburi, mwenye umri wa miaka mitatu.

Basi lashambuliwa, 10 wafariki papo hapo
Mwingine kuondoka Geita Gold FC