Upande wa mashtaka katika kesi ya kusafirisha madini ghafi bila kibali inayomkabili raia wa China, Zhang Chuaqi, wameshindwa kumsomea upya mshtakiwa kwa sababu makalimani hakufika.
Mshatakiwa huyo awali alisomewa mashtaka kwa rugha ya kiingereza, lakini alidai haelewi lugha zaidi ya kichina na kupelekea kesi hiyo kuahirishwa kwa ajili ya kumleta mkalimani.
Hata hivyo, jana mkalimani hakufika mahakamani hapo na Hakimu mkazi mkuu, Salum Ally anayesiliza shauli hilo alikuwa na udhuru hivyo mshtakiwa alipanda kizimbani mbele ya hakimu mkazi Vicky Mwaikambo.
Wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simoni, alidai kuwa shauri lilipelekwa kwa ajili ya mshatakiwa kusomewa mashtaka upya, lakini mkalimani waliyemtegemea hakufika na hakimu aliyesikiliza shauri hilo ana udhuru hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Mwaikambo aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 31 mwaka huu na mshatakiwa alirudishwa rumande.
Mshatakiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili mabayo ni kukutwa na madini na kusafirisha bila kibali.
Imeelezwa kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Desemba 14 mwaka huu eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam ambapo alikutwa anasafirisha madini aina ya amethst bila kibali.
Shitaka la pili mshtakiwa anadaiwa kuwa siku hiyo alikutwa akimiliki madini hayo bila kibali yenye jumla ya uzito wa gram 239 yanye thamani ya dola 369.95 za Marekani sawa na Tsh.851,051.48/=.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo wakili wa utetezi Kelvin Makebula alidai mshatakiwa haelewi lugha ya kiswahili wala kiingereza hivyo anaomba tarehe ya karibu ili mshatakiwa aletewe mkalimani wamsomee upya.
Pia alidai tayari wapo kwenye mazungumzo katika ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) kukiri kosa.