Kiungo Cleophace Mkandala hakuwa na msimu mzuri aliposajiliwa na Azam msimu uliopita na kupewa Thank You’ hivi karibuni, lakini amekiri japo hakukiwsha, ila kuna amejifunza kupitia uwepa kwake kwenye klabu hiyo.

Mkandala alijiunga na Azam akitokea Dodoma Jiji FC lakini hakuwa na wakati mzuri wa kuonyesha kiwango chake, kutokana na nafasi yake kuwepo wachezaji ambao viwango vyao vilikuwa juu.

Mkandala amesema mafunzo aliyoyapata ndani ya kikosi hicho yatamsaidia mbele ya safari kwa timu itakayomsajili kwa msimu ujao, japo hakuweka bayana atatua wapi.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa na wachezaji wenye viwango bora na wenye ushindani na kila mmoja alikuwa anapambania kucheza, sasa aliyekuwa akipata nafasi hawezi kufanya mchezo dakika anazopewa ili kumshaishi kocha,” amesema Mkandala aliyeichezea pia Prisons.

Amesema kwa muda wa mwaka mmoja aliotumika Azam FC, imempa madini mengi akiitazama kazi yake kwa mapana na kuongeza bidii zaidi akiamini bado ana muda wa kufanya makubwa.

“Hilo linatokana na kukutana na wachezaji wanaotazama mbali, hivyo tulikuwa tunabadilishana mawazo ya hapa na pale na nimeondoka nikiwa nimebeba madini ya kutosha,” amesema Mkandala

Ruvu Shooting hatarini kupigwa bei
Kocha Nkoma atoa ushauri wa bure WPL