Waziri wa maji, Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Eng. Nadhifa Kemikimba kumzawadia kiasi cha shilingi milioni moja kama motisha Meneja wa RUWASA Wilaya ya Muleba kwa kubakiza chenji na kuokoa zaidi ya Shilingi 120 millioni.

Aweso ametoa agizo hilo wakati akiwa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera katika ziara yake ya majimbo ya Muleba kaskasini  na Muleba kusini huku akizindua mradi wa maji Rutenge  unaohudumia watu zaidi ya 7000.

Aidha, Waziri Aweso pia  ameagiza kiasi hicho  kilichookolewa kitumike kuwaunganishia maji wananchi ambapo pia alikagua na kuridhishwa na mradi wa maji Katare wenye thamani ya shilingi 3.4 bilioni, unaotarajia kukamilika octoba 2023.

Nao Wabunge wa Majimbo ya Muleba Kaskazini, Charles Mwijage na Muleba Kusini Dkt. Kikoyo wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya Maji Wilayani humo na kupongeza dhamira ya kumtua Mama ndoo kichwani inavyotekelezwa kwa vitendo.

Mvutano waibuka zuio Wanawake kusafiri bila Mwanaume
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 24, 2023