Mkandarasi wa Jengo Jipya la Wizara ya Madini Shirika la Nyumba la Taifa – NHC, ametakiwa kuongeza kasi ili kukamilisha jengo hilo kwa wakati.
Rai hiyo, imetolewa leo Juni 13, 2023 na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Hadi kukamilika kwake Jengo hilo litagharimu shilingi bilioni 22.8 na linatarajiwa kukabidhiwa ifikapo mwezi Septemba, 2023.
Wengine walioshiriki katika ziara hiyo ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ( GST) Dkt. Mussa Budeba, Kaimu Katibu Mtendaji wa TEITI Joseph Kumburu na watumishi wa Wizara ya Madini.