Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amesema katika kipindi cha miaka 10 alichoishi Ikulu, kulifanyika mabadiliko ya fedha mara mbili, na katika kipindi hicho pia Benki kuu ya Tanzania ilitoa noti za sh 5,000 na 10,000.
Katika kitabu chake cha “My Life, My Purpose” amebainisha kuwa aliweka rekodi ya kuwa Rais wa kwanza kwa sura yake kutowekwa kwenye fedha.
Mabadiliko hayo walifanyika mwaka 1997, wakati ilipoondolewa picha ya Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na badala yake ikawekwa picha ya Twiga.
amebainisha kuwa jambo lililo msukuma aweze kufanya uamuzi huo, ni kutokana na tabia yake ya kutopenda kujichukulia kuwa mtu muhimu kuliko wengine.
Halima Mdee ajisalimisha Polisi, aswekwa rumande
Hata hivyo amesema lilikuwa jambo zuri zaidi kwa picha za waasisi wa taifa, Mwalimu Nyerere na Abeid Karume ndizo ziendelee kutumika kwenye fedha.
lakini ameeleza pia aliamua kuchukua uamuzi huo ili kuepusha gharama za kubadilisha noti na sarafu kila mara kwani ingebidi kila utawala unapo badilika na fedha zinabadilishwa.
Mkapa anakumbukwa katika utawala wake kufanya kazi kubwa ya kufufua uchumi na kurejesha imani kwa mataifa wahisani.
Ikumbukwe kuwa, Tanzania alianza kutumia fedha yake yenyewe kwa mara ya kwanza mwaka 1966 na kabla ya hapo ilikuwa inatumia fedha moja na nchi za Kenya na Uganda.