Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amepaza sauti kuwatahadharisha watu waliojitokeza kuwania ngazi mbalimbali za uongozi katika serikali kuzichunga kauli zao.

“Taifa likiwa linaelekea kwenye uchaguzi Mkuu, naomba niwatahadharishe watu wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi kuangalia kauli zao wanapopita kwa wananchi, tusije kuvuruga amani yetu,” alisema Mkapa.

Mkapa alitoa kauli hiyo mwisho mwa wiki iliyopita akizungumza kwenye kilele cha maadhinimisho ya miaka 19 ya radio Maria Tanzania yaliyofanyika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Madhabau ya Bikira Maria jijini Mwanza.

Mkapa aligusia pia suala la Afrika kujipanga na kujiwezesha kwa kutumia mambo yaliyo ndani ya uwezo wao ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha inajitegemea badala ya kutegemea misaada ya wahisani.

Davido Na Diamond Kuperform Pamoja Kwenye Tuzo za MTV/MAMA 2015
CECAFA Yatangaza Ratiba Ya Kagame 2015