Jubilei ya kutimiza miaka hamsini ya ndoa ya rais mstaafu Mh.Benjamin Mkapa jana iliwakutanisha viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikali ambao kwa namna moja ama nyingine imekua ni vigumu kukutana kulingana na vugu vugu la kisiasa linaloendelea hapa nchini.

Jubilei hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Cleopa Msuya, Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba na na waziri mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya ufisadi wa richmond ndg. Edward Lowassa.

Aidha Misa hiyo Takatifu ya Shukrani iliongozwa  na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Askofu Josephat Lebulu na kuhudhuriwa  na Maaskofu Wakuu saba akiwemo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa misa hiyo Rais Magufuli alisema miaka 50 ya ndoa ya Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa Katoliki na Mkewe Mama Anna Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa la Kilutheri inawafundisha watanzania wote hususani wanasiasa kuishi kwa upendo na kuilinda amani waliyonayo na ametoa wito kwa viongozi dini kuendeleza juhudi zao za kuliombea taifa na kuwaunganisha wananchi licha ya tofauti walizo nazo.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa pamoja na kuwashukuru Viongozi wote, ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria Misa hiyo ya Jubilei  ya miaka 50 ya ndoa yake amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijaalia ndoa yake umri mrefu.

Hata hivyo Rais Mstaafu Benjamin Mkapa pia ametoa wito kwa watanzania kupendana na kushirikiana huku akibainisha mafunzo aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa dini kuwa “Kila mmoja ni zawadi kwa mwenzake”
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amempongeza Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna kwa kuadhimisha miaka 50 ya ndoa na amewasihi watanzania kuiga mfano mwema uliooneshwa na wana ndoa hao ambao wamedumu katika imani bila kuyumba.

Chadema Wakanusha Kuhusu Video Zinazozagaa Mitandaoni,Zikionyesha Maandalizi Ya Septemba 1
Jeshi La Polisi Kanda Maalumu Ya Dar es salaam Laongeza Nguvu Operesheni Ya Vikindu,La peleka Askali Wengine 80,Taarifa Kamili Kutolewa Jumanne