Dili ya H Baba kujiunga na klabu ya Toto ya Mwanza imepata kizuizi na huenda mwimbaji huyo wa Bongo Flava akashindwa kuendelea na ndoto yake hiyo.

Kwa mujibu wa H-Baba, Mkewe Flora Mvungi ameweka pingamizi kwa uamuzi wake na anamtaka arudi Dar es Salaam ili wawe karibu zaidi kama familia.

Mkali huyo wa ‘Mpenzi Bubu’ ameeleza kuwa mkewe yuko serious katika hilo na tayari wameshakaa vikao vya familia na ndugu wa pande zote kumshawishi abadili uamuzi wake.

“Unajua wife anacholalamika kuwa nitakuwa mbali na familia, kwahiyo atakosa haki haki yake ya msingi kama mke,” alisema H-Baba.

Alisema kuwa endapo mkewe ataweka msisitizo katika hilo ataachana na ndoto ya kuendelea kuichezea klabu hiyo.

H-Baba ni mwimbaji, Mchezaji wa muziki (dancer) aliyebarikiwa uwezo mkubwa wa kucheza mpira wa miguu kama ilivyo kwa wasanii wengine wa Bongo Flava kama Ali Kiba na Hussein Machozi.

Wenyeviti Wengine Wa CCM Watimkia Chadema
Hisia Za Manyanyaso Ya kijinsia Zaibuka