Mke wa Nahodha na Mshambuliaji wa kikosi cha Tottenham Harry Kane ameoneka na Jijini Munich nchini Ujerumani na taarifa zinadai yupo huko kwa ajili ya kuangalia nyumba na shule kwa ajili ya watoto wao kabla mumewe hajakamilisha uhamisho wa kujiunga na FC Bayern Munich kwenye dirisha hili.

Kane mwenye umri wa miaka 29, anadaiwa kuweka wazi kwamba ahitaji tena kuendelea kusalia Tottenham kwa msimu ujao 2023/24.

Munich inadaiwa kuwa kwenye hatua za mwisho kuwasilisha ofa ya Pauni 100 milioni ili kumsajili Kane baada ya majadiliano ya muda mrefu na mabosi wa Spurs.

Wababe hawa wa Ujerumani wanadaiwa kuwa waliwasilisha ofa mbili zilizokataliwa ikiwa ile ya kwanza ya Pauni 60 milioni na ile ya Pauni 70 milioni.

Licha ya Kate ambaye ndio mke wa Kane kuonekana Jijini humo, Kane mwenyewe kwa sasa yupo na kikosi cha Spurs barani Asia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Luis Miquissone azua gumzo zito Simba SC
Hatma ya Tshishimbi mikononi mwa Kopunovic