Mke wa Rais wa zamani wa Zambia Esther Lungu ambaye mumewe ni Edgar Lungu, amehojiwa na Wakala wa Kupambana na Utakatishaji Fedha wa Zambia kuhusu umiliki wake wa nyumba 15 za kisasa zilizopo katikati ya Mji wa Lusaka.
Nyumba hizo 15 mwanzo wa mwezi Julai ziliwekwa chini ya uangalizi maalum na Tume ya Udhibiti Madawa ya nchini humo zikidhaniwa kuwa zilipatikana kijinai.
Wakala wa Kupambana na Utakatishaji Fedha wa Zambia ilishikilia nyumba hizo ya baada ya Esther kusema anazimiliki.
Akimabatana na Mumewe Edgar Lungu na Mawaziri kadhaa wa zamani Esther alikwenda kuhojiwa na Watoto wawili wa Lungu pia walihojiwa kuhusu tuhuma za rushwa.
Familia nzima ya Rais huyo wa Zamani imewekwa kwenye viuizi vya tume za Upelelezi Zambia Ingawa Serikali ya Rais wa sasa Hakainde Hichilema imekuwa ikikosolewa na baadhi ya wachambuzi kuwa inafanya matukio hayo kwa sababu za kisiasa.
Rais huyo wa sasa ambaye aliingia madarakani mwaka jana Agosti aliahidi kuwa kurudisha mali zote za Lungu ambazo zimepatikana kwa njia zisizo halali.