Sylvia Bongo Ondimba Valentin ambaye ni mke wa Rais aliyeondolewa madarakani Nchini Gabon, Ali Bongo Ondimba, amefungwa jela kwa kupatikana na hatia ya utakatishaji wa fedha na kughushi nyaraka.

Kwa mujibu wa taarifa za Wakili wake, Francois Zimeray ambaye hakutaja ni kifungo cha aina gani, amesema analaani hukumu hiyo iliyotolewa kiholela na isiyofuata utaratibu rasmi na kanuni za vifungo kwa mteja wake ambaye alishitakiwa Septemba 28, 2023.

Sylvia na mumewe Ali Bongo enzi za furaha.

Sylvia amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu kulipotokea mapinduzi mwishoni mwa mwezi Agosti 2023 na alikuwa akituhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma.

Viongozi wa mapinduzi wamekuwa wakimtuhumu Bongo na wapambe wake, kwa kughushi matokeo ya uchaguzi na pia walimtuhumu Sylvia na mtoto wake wa kiume, Nourredin Bongo Valentin kwa kumlaghai ili wafanikishe mipango yao.

Ulinzi, Uhalifu: Wafanyabiashara watakiwa kutoa ushirikiano
Mahakama yafuta kesi uingizaji, ulimaji mazao Kijenetiki